Nafaka:
Nafaka ni vyakula vya punje punje au chembechembe
kama vile mtama, mahindi, ngano, uwele (mawele),
mpunga n.k. Virutubisho vya msingi vinavyopatikana
katika vyakula vya nafaka ni wanga, sukari na nyuzi
nyuzi. Virutubisho vya ziada ni Protini, vitamini
(kundi la B) na baadhi ya madini.
Vyakula jamii ya mizizi na matunda
Vyakula jamii ya mizizi (starchy roots) ni kama vile
viazi (vitamu, mviringo, n.k) mihogo, n.k. Virutubisho
vya msingi vinavyopatikana katika vyakula jamii ya
viazi na matunda ni wanga, sukari na nyuzi nyuzi
(dietary fibres). Zaidi ya virutubisho hivyo ni baadhi
ya madini, vitamini C (kama chakula hicho siyo
kikavu) na vitamini A (kama chakula hicho kinarangi
ya njano).
Vyakula jamii ya maharage
Vyakula jamii ya maharage nikama vile maharage ya
kawaida na yale ya soya, kunde, choroko, n.k.
Virutubisho vya muhimu katika kundi la vyakula vya
hapo juu ni wanga, protini na nyuzi nyuzi.
Virutubisho vya ziada ni vitamini (kundi B) na
madini.
Mbegu za mafuta
Mbegu za mafuta ni kama vile alizeti, pamba, ufuta,
nazi, mawese (chikichi), kweme, maboga, tikiti maji,
matango, n.k.
Virutubisho vinavyopatikana kwa wingi katika mbegu
za mafuta ni mafuta, protini na nyuzi nyuzi. Ziada
kundi B. (B- Vitamins).
Nyama/Samaki
Virutubisho vya msingi katika nyama au samaki ni
protini, mafuta na madini ya chuma. Virutubisho
vingine ni vitamini vya kundi B na madini (zaidi ya
yale ya chuma).
Ini
Ini linatupa virutubisho vya msingi vya protini,
madini ya chuma na vitamini.
Maziwa
Virutubisho tunavyovipata kwa wingi katika maziwa
ni mafuta, protini, baadhi ya madini na vitamini.
Mayai
Mayai yana virutubisho vya msingi vya protini na
vitamini. Zaidi ya hivyo ni mafuta na madini (siyo ya
chuma).
Mafuta
Mafuta kama chakula yanatupa mafuta kama
kirutubisho cha msingi. Zaidi ya hicho ni uwezekano
wa kupata vitamini A.
Mboga za majani
Mboga za majani hasa zile za kijani zinavirutubisho
vya msingi vya vitamini A, C na B, Zaidi ya hivyo ni
protini, madini na nyuzi nyuzi.
Matunda jamii ya machungwa
Matunda jamii ya machungwa ni machungwa,
machenza, n.k virutubisho vya msingi tunavyovipata
kutoka katika matunda jamii ya machungwa ni sukari,
vitamini A na C. Zaidi ya hivyo ni madini na nyuzi
nyuzi.
Sunday, 10 August 2014
VIRUTUBISHO VINAVYOPATIKANA KATIKA VYAKULA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment