SHINIKIZO LA DAMU AU PRESHA
Shinikizo la damu au presha ambalo kitaalamu huitwa Hypertension au High Blood Pressure ni neno la kitiba linalotumika kueleza hali ya ugonjwa wa shinikizo la juu la damu. Shinikizo la damu ni muhimu kwa ajili ya kusukuma damu katika sehemu zote za mwili, lakini shinikizo la damu la juu huweza kuleta matatizo na madhara makubwa kiafya. Shinikizo la damu kwa kawaida husababishwa na kuongezeka msukumo wa damu katika kuta za mishipa ya damu, hali ambayo huufanya moyo ufanye kazi zaidi kuliko kawaida ili kuzungusha damu mwilini. Shinikizo la damu huanishwa na namna damu inavyopiga kwenye kuta za mishipa ya damu. Kwa kawaida shinikizo la damu la mtu hupanda na kushuka kila siku, kwa baadhi ya watu hubakia juu na hapo ndipo huambiwa kuwa wana shinikizo la juu la damu. Ugonjwa huu kwa kawaida huitwa muuaji wa kimya kimya kwa maana kuwa, mtu anaweza akawa na ugonjwa huo kwa miaka kadhaa lakini bila kujua, huku ugonjwa huo ukimletea madhara makubwa. Njia ya pekee ya kujua iwapo una ugonjwa huu, ni kwenda kupimwa shinikizo lako la damu. Hii ni kwa sababu shinikizo la damu lisilodhibitiwa huathiri na kuharibu moyo, macho na figo na huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa moyo na kiharusi.
Shinikizo la damu au presha huonyeshwa kwa muhtasari wa vipimo viwili vya sistoli na dayastoli, ambapo sistoli ni kipimo cha damu kinachopima nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa ya damu wakati moyo ukidunda, na diyastoli ni kipimo cha damu kinachopima nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa ya damu wakati moyo umepumzika au kati ya mapigo ya moyo. Shinikizo la damu hupimwa katika milimeta mercury. Kiwango cha kawaida cha msukumo wa damu pale mwili unapokuwa haupo katika harakati huanzia sistoli 100 hadi 140 mmHg na diyastoli 60 hadi 90 mmHg. Shinikizo la juu la damu ni pale vipimo hivyo vinapozidi mmHG 140/90.
&&&&&&&&
Shinikizo la damu limegawanyika katika makundi mawili, ambayo ni
ENDELEA KUSOMA BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment