Saturday, 26 July 2014

UGONJWA WA FIGO


Figo
Magonjwa ya figo

Figo hufanya kazi muhimu mwilini ambazo ni:-
• Kudhibiti na kuhifadhi virutubishi na maji na kuondoa mabaki kupitia mkojo.
• Kuchuja damu ili kuondoa mabaki ambayo ni sumu mwilini. Baadhi ya mabaki hayo ni urea, uric acid, creatinine na ammonia.
• Kudhibiti viwango vya electrolyte mwilini, yaani Sodium (Na+ ) na Potassium (K+). Sodium husaidia kudhibiti wingi wa maji mwilini na pia huwezesha mawasiliano kati ya mfumo wa fahamu na misuli (enhances commucacation between brain/nerves and muscles).Potassium husaidia mapigo ya moyo between brain/nerves and muscles). Potassimu husaidia mapigo ya moyo (regulates heart beats) na kazi ya misuli (muscle function). Viwango vya kawaida kwa Sodium ni 135-145 mmol/L na Potassimu ni 3.5-5 mmol/L.
• Kudhibiti shinikizo la damu kupitia mfumo wa rennin-angiotension.
• Kutengeneza kichocheo cha Erythropoietin ambacho huchochea utengenezaji wa chembechembe nyekundu za damu.
• Kuchochea vitamin D ambayo hutumika katika kudhibiti kiwango cha Calcium na Phosphorous kwenye mifupa.

No comments:

Post a Comment